Dodoma FM

TBS na WMA watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu

12 January 2021, 7:48 am

Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe amewataka watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya kazi kwa uadilifu na kuwafikiria wafanya biashara wakati wakitoa huduma ili kuendelea kutengeneza taswira nzuri ya bidhaa  za Tanzania katika soko la ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe

Waziri Mwambe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na menejimenti na wafanyakazi wa TBS na WMA alipofanya ziara katika  taasisi hizo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda Mhe. Exaud Kigahe pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara katika taasisi hizo.Akiwa TBS, Waziri Mwambe ameiagiza TBS kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa kushirikiana na taasisi nyingine  zinazohusika na ukaguzi wa mizigo bandarini  na mipakani ili kupunguza muda unaotumika kukagua bidhaa hizo,kupunguza mianya ya rushwa na kurahisisha utoaji wa mizigo hiyo kwa haraka.