Dodoma FM

Wakazi wa Ndachi watarajia ahueni ya migogoro ya ardhi baada ya zoezi la upimaji kukamilika

12 August 2021, 11:48 am

Na; Mariam Matundu.

Kufutia mgogoro wa ardhi wa muda mrefu katika Mtaa wa Ndachi Jijini Dodoma hatimae wakazi wa Mtaa huo wanatarajia kupata ahuweni kutokana na kukamilika kwa upimwaji wa viwanja.

Taswira ya habari imezungumza na mwenyekiti wa mtaa huo Bi. Joyce Habeli na kueleza kuwa wanatarajia kuanza zoezi la ugawaji wa viwanja kwa wananchi wa mtaa huo mnamo mwezi September mwaka huu .

Aidha amekutoa angalizo kwa watu wanaoenda kununua viwanja mtaani hapo kwani kumekuwa na wimbi kubwa la matapeli wanaouza viwanja ambavyo sio vya kwao hasa katika kipindi hiki ambapo bado ugawaji wa vijanja haujafanyika.

Mtaa wa Ndachi umekuwa ukiandamwa na migogoro ya ardhi kwa muda mrefu sasa ambapo kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa huo migogoro hiyo inaenda kumalizika.