Dodoma FM

Bahi Sekondari wamshukuru Rais Samia

1 May 2023, 4:28 pm

Frank Mcharo Mkuu wa Shule Bahi Sekondari. Picha na Bernad Magawa.

Amewaomba viongozi hao kusaidia kutoa elimu ili wazazi wachangie chakula cha mchana kwa watoto jambo ambalo litasaidia kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo.

Na Bernad Magawa.

Uongozi wa Shule ya sekondari bahi umetoa shukrani kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kutoa zaidi ya Millioni 200 kujenga madarasa shuleni hapo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa shule hiyo Frank Mcharo alipotembelewa na Uongozi wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Bahi kuona maendeleo ya kitaaluma katika shule hiyo huku akiwaelezea viongozi tatizo la kukosekana kwa uzio shuleni hapo hali inayoleta ugumu katika kuwakabili wanafunzi kutokana na shule hiyo kuwepo eneo la mjini.

Sauti ya Mkuu wa shule
Muonekano wa Shule ya sekondari Bahi Sokoni. Picha na Bernad Magawa.

Nao viongozi wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Bahi walipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi shuleni hapo na kuwasisitiza kutumia fursa ya uwepo wa majengo mazuri shuleni hapo kusoma kwa bidii ili elimu watakayoipata iwasaidie kuendesha maisha yao ya baadaye.

Sauti za Viongozi wa Jumuiya ya wazazi.

Awali akizungumza na viongozi wa jumuiya ya wazazi Ofisini kwake Mwalimu Mcharo alieleza ushirikiano mdogo anaoupata kutoka kwa wazazi wenye watoto shuleni hapo .