Dodoma FM

Marufuku uvutaji wa sigara hadharani

2 May 2024, 6:03 pm

Ifikapo mwaka 2030 vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigara vitaongezeka kufika zaidi ya watu milion 8 kila mwaka.

Matumizi ya sigara yana athari nyingi za kiafya kwa matumizi ya binadamu kwani ina Kemikali zaidi ya 4000 na 40 zikiwa ni hatari zaidi kwa kusababisha Magonjwa ya Saratani kwa Wanaume na Wanawake.

Na Mindi Joseph.
Wananchi Mkoani Dodoma wamepongeza serikali kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani.
Uvutaji wa sigara hadharani umekuwa na athari kwani Kwa mujibu wa Wizara ya Afya inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030 vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigara vitaongezeka kufika zaidi ya watu milion 8 kila mwaka.

Tayari Bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ambayo imetoa katazo la uvutaji wa sigara hadharani na hapa wananchi wanasema.

Sauti za wananchi
Matumizi ya sigara yana athari nyingi za kiafya kwa matumizi ya binadamu kwani ina Kemikali zaidi ya 4000 na 40 zikiwa ni hatari zaidi

Sheria hiyo imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali hapa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel anabainisha hayo.

Sauti ya Naibu waziri wa Afya.