Dodoma FM

Wakazi wa Miganga waiomba serikali kuendelea kusambaza umeme

18 October 2022, 6:10 am

Na; Benard Filbert.

Wakazi wa kijiji cha Miganga Kata ya Idifu wilaya ya Chamwino wameiomba serikal kuendelea kusambaza nishati ya umeme katika kijiji hicho hali itakayosaidia kukua kwa uchumi.

Ombi hilo wamelitoa wakati wakizungumza na Taswira ya habari kuhusu uwepo wa nishati ya umeme umekuwa  na fursa gani kwa wakazi wa kijiji hicho.

Wananchi hao wameiambia taswira ya habari kuwa awali vijana wengi walikuwa wanahama kijijini hapo kutokana na ukosefu wa umeme lakini hivi sasa wengi wao wamejiajiri.

Pia wamesema ni vyema serikali ikaendelea kusambaza umeme maeneo ambayo huduma hiyo haijafika ili kumfikia kila mwananchi.

.

John Mawaya ni mwenyekiti wa kijiji hicho ameshukuru baadhi ya maeneo katika kijiji chake kufikiwa na umeme huku akisema bado anawasiliana na shirika la Umeme kuhakikisha wanafikisha huduma hiyo katika maeneo yote.

.

Kufikishwa kwa huduma ya umeme kwa maeneo ya vijijini nchini imesaidia wakazi wengi wa maeneo hayo kujiajiri na kukuza uchumi wa eneo husika.