Dodoma FM

Wananchi Wilayani Kongwa wanavyoshiriki kutunza mazingira

2 December 2020, 8:38 am

Moja ya Misitu iliyotunzwa kwa uoto wa asili

Na Selemani Kodima

Dodoma.

Ushirikiano wa wananchi na Uongozi wa Kijiji cha Sejeli Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma umetajwa kama njia inayoweza kukomesha uharibifu wa mazingira hususani ukataji wa Miti hovyo.

Hayo yanajiri baada ya hivi karibuni Uongozi wa Kijiji cha Sejeli kuwakamata watu wawili ambao walikuwa wakikata miti katika eneo ambao limetengwa kwa ajili hifadhi ya mazingira.

Akizungumza na Taswira ya habari Mwenyekiti wa Kijiji cha Sejeli Bw.Amos Mazengo amesema kutokana na juhudi kubwa ambazo wamekuwa wakizifanya zimesaidia kuwapa msukumo wananchi kutoa ushirikiano pale wanapobaini mtu anaharibu mazingira.

Bw.Mazengo amesema kuwa kupitia elimu ya utunzaji wa mazingira kwa njia ya kisiki hai imekuwa mkombozi ndani ya Kijiji chake na imesaidia kuleta mabadiliko chanya katika Mazingira.

Hata hvyo njia ya kisiki hai ambayo imekuwa ikitumiwa na baadhi ya wananchi Kijijini hapo ni mojan ya njia ya kutunza maotea ya miti yanayochipua kutokana na kisiki hai au mbegu za miti zilizodondoshwa ardhini na vinyesi vya wanyama au ndege.