Dodoma FM

Homa ya ini yaelezwa kuua idadi kubwa ya watu Duniani kila mwaka.

29 July 2021, 9:25 am

Na;Mindi Joseph.

picha ya inni.

Takribani watu 88,4000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya homa ya ini kwa mujibu wa Takwimu za shirika la afya Duniani.

Kupitia taarifa ya Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto iliyotolewa kwa vyombo vya habari ina ainisha kuwa ugonjwa huu ni hatari na unaoua idadi kubwa ya watu polepole kwani kati ya watu 100 watu 8 wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huo na inakadiriwa kila baada ya dakika mbili watu wawili hufariki duniani kutokana na homa ya ini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Mratibu wa Homa ya Ini kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Dr Baraka Nzobo amesema kundi la watu wanaojidunga dawa za kulevya,wanywaji wa pombe kupita kiasi ni miongoni mwa makundi ambayo yako hatarini kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha Dkt Nzobo amesema kuwa tafiti zilizofanyika nchini zinaonesha kuwa Tanzania ina asilimia 4 za wagonjwa wa homa ya ini na amewasihi wazazi wote kuhakikisha Mtoto anapozaliwa anapata chanjo zote ili kumlinda na ugonjwa huo na magonjwa mengine.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya Homa ya Ini Duniani Huadhimishwa kila ifikapo Julai 28 ya kila mwaka na Takwimu kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama zinaonesha Mikoa iliyokuwa na maambukizi makubwa ya Homa ya Ini kwa mwaka 2020 kwenye kundi la watu wanaochangia damu ni Mara (9.3%),Geita (8.7%),Morogoro(7.7%),Rukwa(7.6%) na Shinyanga (7.4%)

Maadhimisho yamwaka huu yanakwenda sambama na kauli mbiu isemayo ‘’Tusisubiri Kupima Kuanza Matibabu na kupata chanjo ya Homa ya Ini’.