Dodoma FM

Wananchi waaswa kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa zoezi la Sensa

11 July 2022, 1:30 pm

Na; Benard Filbert.

Kuelekea zoezi la sensa ya watu na makazi linalo tarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu wakazi wa kata ya Songambele Wilayani Kongwa wameombwa kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu badala yake wawape fursa ya kuhesabiwa.

Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Songambele bwana Patrick Inveso wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu utayari wa wananchi kuelekea zoezi la sensa na makazi.

Amesema ni vyema jamii ikazingatia kuwa sensa ni zoezi muhimu kwakila mtu hivyo kila mtu anatakiwa kuhesabiwa.

.

Kadhalika ameongeza kuwa elimu hiyo wamekuwa wakiitoa katika mikutano ya hadhara ambayo wamekuwa wakiifanya kwa lengo la kuondoa mitazamo hasi ambayo ipo kwenye jamii kuhusu suala la sensa.

.

Sensa ya watu na makazi inatarajiwa kufanyika agosti 23 mwaka huu ili kupata takwimu sahii ya watu na makazi kwa maendeleo ya nchi.