Dodoma FM

Wakazi wa Fatina walalamika maji taka kutiririka mtaani

2 August 2023, 3:43 pm

Picha ni chemba zinazopita katika mtaa huo wa Fatina zikiwa zinatiririsha maji taka hayo. Picha na Yussuph Hassan.

Hivi karibuni kumekuwa na changamoto ya kuzibuka kwa chemba za maji taka na kutiririsha maji katika mtaa wa Fatina, ambapo kwa mujibu wakazi wa eneo hilo chemba hizo huchukuwa takribani hadi muda wa siku 10 katika kuzibuliwa.

Na Mariam Msagati.

Wananchi wa kata Majengo mtaa Fatina jijini Dodoma wamelalamikia changamoto ya kuzibuka mara kwa mara kwa chemba za maji taka na kutiririsha maji mtaani.

Wakizungumza na Dodoma TV wakazi hao, wamesema kuwa changamoto hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara suala ambalo limekuwa linahatarisha afya zao na biashara kwa ujumla.

Sauti ya wakazi .
Changamoto hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara suala ambalo limekuwa linahatarisha afya zao. Picha na Yussuph Hassan.

Aidha wameiomba Serikali kumaliza changamoto hiyo kwani imekuwa ni tatizo linalojirudia.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mweyekiti wa Mtaa wa Fatina amesema kuwa changamoto hiyo tayari inashughulikiwa na wataalam kutoka DUWASA huku akibainisha chanzo cha changamoto hiyo.

Sauti ya mwenyekiti .