Dodoma FM

Faundation for civil society yajadili utoaji huduma bora za kijamii

16 March 2022, 2:06 pm

Na;Mindi Joseph .

Taasisi ya Foundation for civil society Leo imekutana na wadau wa habari Kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma bora za kijamii kwa wananachi.

Akizungumza na Taswira ya Habari Afisa Program Mwandamizi Nicolaus Mhozya amesema lengo la kukutana na wanahabari ni kutoa mchango wao ambao utakuwa na tija kwa Jamii.

Ameongeza kuwa Kituo cha AZAKI kinaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wengine na kutoa elimu ya uzingatiaji wa sheria.

Amebainisha kuwa Walengwa wakuu ni  watunga sera wananchi kwa ujumla kwa kushirikiana na wadau  wote katika kuleta maendeleo nchini.

Ikumbukwe kuwa jamii inahaki ya kupata huduma bora za kijamii katika nyanja mbalimbali .