Dodoma FM

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa

8 June 2022, 2:28 pm

Na; Lucy Lister .

Vijana jijini Dodoma wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza na kuacha tabia ya kuchagua  kazi.

Akizungumza na Dodoma fm Bw. Charles Mathias ambaye anajishughulisha na suala la kuongeza thamani kupitia biashara ya kuku ambae hapa anaelezea namna biashara ya kuku ilivyomsaidia katika suala la kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wakabainisha hali ya biashara ilivyo kwa sasa huku wakieleza mbinu wanazozitumia katika kudhibiti kuku hao kuambukizana magonjwa mbalimbali yanayojitokeza.

.

Shughuli ya kuuza, pamoja na kuongeza thamani ya kuku katika soko la mwembeni jijini Dodoma imeendelea kuwa fursa kwa vijana mbalimbali jijini hapa kutokana na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ya umasikini.