Dodoma FM

Kata ya Chiwe yakusanya fedha kwaajili ya ujenzi wa sekondari Moleti

27 September 2021, 12:15 pm

Na; Benard Filbert.

Serikali ya kata ya Chiwe wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma imefanikiwa kukusanya zaidi ya milioni 30 lengo ikiwa kujenga shule ya sekondari moleti ili kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Chiwe Bwana Dastan Limaoga wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya elimu ya sekondari katika kata ya Chiwe.

Bwana Dastan ameiambia taswira ya habari kuwa kata ya Chiwe inashule 7 za msingi ambazo wanafunzi wakihitumu darasa la saba wanakuwa wengi kutokana na uwepo wa shule moja ya sekondari ambayo haikidhi idadi kubwa ya wanafunzi wanapofanikiwa kujiunga na shule hiyo.

Hata hivyo amewapongeza wakazi wa kijiji cha moleti kwa kuwa mstari wa mbele kutoa michango kwani hadi hivi sasa wamechanga milioni 21 tofauti na vijiji vingine.

Hata hivyo amesema baada ya muda mfupi watakamilisha ujenzi wa shule hiyo huku akisema itapunguza kero ambayo wanafunzi wamekuwa wakikutana nayo hususani kipindi cha mvua.
Kata nyingi zimekuwa zikikabiliwa na uhaba wa shule za sekondari huku wanafunzi wakitembea umbali mrefu kufuata shule kwa ajili ya masomo.