Dodoma FM

Tanzania yaahidi kuendeleza ushirikiano na India

29 November 2021, 1:56 pm

Na; Fred Cheti.

Serikali imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya Uganda katika mambo mbalimbali ikwemo katika masuala ya elimu na biashara ili kuendelea kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo.

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia mbele ya Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni pamoja na Mamia ya wananchi waliojitokeza wilayani Chato Mkoani Geita katika uzinduzi wa shule ya Museveni iliyojengwa wilayani humo chini ya ufadhili wa serikali ya Uganda.

CLIP 1 …RAIS SAMIA CHATO

Kwa upande wake Rais wa Uganda Mh. Yoweri Museveni aliyewasili nchini Novemba 27 amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo moja ya matokea ya undugu na ushirikiano ulipo kati ya nchi hizo mbili ambapo amesema kuwa serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuleta maendeleo zaidi baina ya nchi hizo.

CLIP 2…. RAIS MUSEVENI CHATO

Katika hatua nyingine Rais Samia amewataka watanzania kuacha kuibua mijadala isiyokua na msingi juu ya uamuzi wa serikali wa kuwarudisha wanafunzi walioshindwa kumaliza masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito kwani uamuzi huo unatoa fursa pana kwa watoto hao kuweza kuendelea na masomo.

CLIP 3..RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo wamefanya uzinduzi wa Shule ya Msingi Museveni iliyopo Wilaya ya Chato, Mkoani Geita ambayo imejenwa chini ya Ufadhili wa seriakli ya Uganda.