Dodoma FM

TBS yasisitiza wadau kushiriki uandaaji wa viwango

18 October 2023, 1:47 pm

Picha ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa TPSF Bw. Gaspa Kahungya akizungumza na waandishi wa habari.Picha na mtaa kwa mtaa.

Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania, TBS, Shirika la Viwango Zanzibar, ZBS pamoja na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), imeandaa tuzo za ubora za kitaifa awamu ya nne kwa 2023 kwa wajasiriamali, wazalishaji wa viwandani na watoa huduma.

Na Mindi Joseph.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuwahimiza  wadau kushiriki katika uandaaji wa viwango ili kusaidia  uzalishaji wa bidhaa bora zinazoweza kushindana katika masoko.

Picha ni Afisa ubora mwandamizi wa TBS, Bw.Athumani Kissumo akizungumza na waandishi wa habari .Picha na Mtaa kwa mtaa .

Viwango vinasaidia kupunguza gharama pamoja na kuongezea wateja kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

Meneja wa Viwango Bw.Yona Afrika anasema suala la uandaaji wa viwango linahusisha wadau wote wa uzalishaji wa bidhaa na sio la Shirika la Viwango pekee.

Sauti ya Bw.Yona Afrika .