Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya malaria

13 July 2026, 15:36

Ugonjwa wa malaria ni hatari kwa watoto chini ya miaka mitano.Picha na Mtandao.

Kulingana na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbali mbali kumekuwa na matokeo mazuri ya kupunguza maambukizi.

Na Jerome John.

Jamii mkoani Dodoma imeshauriwa kuendelea kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria.

Wito  huo umetolewa na Dkt. Ally  Olotu,Mkurugenzi wa Sayansi Ifakara  Health Institute akizungumza na Taswira ya Habari juu ya namna gani jamii inaweza kujikinga na ugonjwa huo.

Daktari Ally amebainisha kuwa ugonjwa wa malaria ni hatari kwa watoto chini ya miaka mitano na kwa mama wajawazito hivyo ni vema kuchukua hatua mbali mbali katika kudhibiti na kujikinga hasa kutokomeza mazalia ya mbu yaliyopo katika mazingira yao.

Sauti ya Dkt. Ally  Olotu.

Aidha ameeleza kuwa kulingana na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbali mbali kumekuwa na matokeo mazuri ya kupunguza maambukizi hayo kwa kufanya tafiti mbali mbali zinazo saidia kuleta mbinu mbali mbali zinazo tumiwa katika kutokomeza ugonjwa huo.