Wanawake watajwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa wanaume
30 July 2026, 17:40

Wanandoa kujenga utamaduni wa mawasiliano ya wazi, kuheshimiana na kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo, huku akisisitiza umuhimu wa kutafuta ushauri wa kitaalamu mapema ili kuzuia msongo wa mawazo na mfadhaiko usiathiri afya ya akili na ustawi wa familia.
Na Daniel Njau.
Wanaume wameeleza kuwa baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika ndoa na familia zimekuwa zikichangia kupata msongo wa mawazo na hata kufikia hali ya mfadhaiko.
Baadhi ya wanaume wamesema licha ya changamoto za kiuchumi, kumekuwepo pia na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya wanawake dhidi ya wanaume, hali inayowaathiri kisaikolojia na kusababisha migogoro ndani ya familia.
Akizungumza kuhusu suala hilo,Bi Janeth Mwambipile mtaalamu wa saikolojia amesema mfadhaiko ni hali inayotokana na mtu kubeba mawazo mengi yanayosababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira, kipato duni, magonjwa pamoja na migogoro ya kifamilia, na kwamba hali hiyo inaweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia.