Adhabu kali kwa watoto huwa athiri kisaikolojia
22 September 2026, 17:17

Adhabu kali hazisaidii kuwafundisha watoto, bali huwajaza hofu na kuwafanya kuwa waoga.
Na Daniel Njau.
Adhabu kali wanazopewa watoto majumbani na shuleni zimetajwa kuwa na madhara katika ukuaji wao wa kisaikolojia, huku wataalamu wakisisitiza matumizi ya njia mbadala za malezi na nidhamu zisizowaathiri watoto kimwili wala kiakili.
Kwa upande wake Mwanasaikolojia, Bwana Sabas Massawe, amesema si lazima mtoto aadhibiwe kwa viboko au kutukanwa kwa kauli zisizofaa, kwa kuwa hatua hizo zinaweza kumsababishia majeraha ya kimwili na kisaikolojia.
Amesema wazazi na walezi wanaweza kutumia njia nyingine za kumfundisha mtoto kutambua kosa alilolifanya na kujifunza kutokana na makosa hayo, badala ya kutumia adhabu kali zinazoweza kuleta hofu.
Baadhi ya wananchi wamesema adhabu kali hazisaidii kuwafundisha watoto, bali huwajaza hofu na kuwafanya kuwa waoga kiasi cha kushindwa kueleza changamoto zinazowakabili, hali inayoweza kuathiri ukuaji na mahusiano yao na wazazi, walezi na walimu.