Dodoma FM

Wafugaji wametakiwa kuchanja mifugo kukabiliana na magonjwa

12 October 2026, 17:50

Picha ni Daktari wa mifugo akiwa katika zoezi la chanjo kwa wanyama. Picha na Joy Fm.

Wafugaji wametakiwa kushirikiana na maafisa wa mifugo kupata ushauri wa kitaalamu na kuhakikisha mifugo yao inapata chanjo, tiba na kinga dhidi ya magonjwa kwa wakati ili kupunguza vifo na hasara katika shughuli za ufugaji.

Na Victor Chigwada.

Wafugaji wametakiwa kuchukua tahadhari mapema kwa kuchanja na kuogesha mifugo yao ili kuzuia magonjwa yanayoweza kuongezeka wakati wa msimu wa mvua unaohusishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Wito huo umetolewa na Afisa Kilimo na Mifugo wa Kata ya Handali, Daudi Kolokoni, aliyesisitiza umuhimu wa kutoa chanjo kwa mifugo ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kujitokeza katika kipindi hicho.

Kwa upande wao, baadhi ya wafugaji wamesema wamekuwa wakipoteza mifugo kutokana na magonjwa yanayoshamiri wakati wa msimu wa mvua, wakieleza kuwa ukosefu wa tiba na dawa za kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na kupe ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili.