Sheria za teknolojia zatakiwa kwenda sambamba na mabadiliko
17 November 2026, 15:25

Hatua hiyo inalenga kuisaidia Tanzania kuwa na mfumo wa kisheria unaoendana na mabadiliko ya teknolojia, ili kuhakikisha matumizi ya Akili Unde yanafanyika kwa kuzingatia uwajibikaji, usalama na haki za wananchi, sambamba na kulinda maslahi ya taifa.
Na Anwary Shabani.
Kasi ya maendeleo ya teknolojia na matumizi ya Akili Unde imeibua tahadhari kuhusu uwezekano wa Tanzania kukabiliwa na mashauri ya kisheria iwapo haitakuwa na mifumo madhubuti ya kisheria ya kudhibiti matumizi ya teknolojia hiyo, huku viongozi wa taasisi wakitakiwa pia kuimarisha uelewa wa usalama wa mtandao.
Dkt. Laltaika ametoa mfano wa shauri lililofunguliwa nchini Kenya dhidi ya Serikali, Mwanasheria Mkuu, Bunge na taasisi nyingine za umma, kutokana na madai ya matumizi ya Akili Unde bila kuwepo kwa mfumo wa kutosha wa kisheria, akieleza kuwa Tanzania inaweza kukumbana na changamoto zinazofanana, ikiwemo katika mahakama za kikanda, endapo haitachukua hatua za mapema.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, George Mandepo, amesema utafiti unaofanywa na Tume hiyo unalenga kubaini mapungufu yaliyopo katika sheria na mifumo ya kitaasisi inayosimamia matumizi ya teknolojia, pamoja na kupendekeza hatua stahiki za kuchukuliwa.