Dodoma FM

Wananchi watakiwa kushiriki mapambano dhidi ya rushwa

5 November 2026, 17:05

Rushwa inaathiri maisha ya kila siku, hususan katika upatikanaji wa huduma muhimu.Picha na michuzi.

Hivyo, mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji ushirikiano wa wananchi, viongozi na taasisi zinazohusika ili kujenga jamii yenye haki, uwazi na maendeleo endelevu.

Na Mwanaid Mpetu.

Rushwa imeendelea kuwa miongoni mwa changamoto zinazokwamisha maendeleo ya jamii kutokana na athari zake katika utoaji wa huduma, usawa na haki kwa wananchi.

Hali hiyo imeelezwa kuchangia kuongezeka kwa gharama za maisha, kupunguza imani ya wananchi kwa taasisi mbalimbali pamoja na kuwanyima baadhi ya watu haki zao za msingi.

Baadhi ya wananchi wanasema rushwa inaathiri maisha ya kila siku, hususan katika upatikanaji wa huduma muhimu.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake, mtaalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Said Suleiman ameeleza kuwa rushwa ina athari kubwa katika maendeleo ya jamii, ikiwemo kudhoofisha uchumi, kuathiri utoaji wa huduma za kijamii na kuvuruga misingi ya haki na uwajibikaji.

Sauti ya Said Suleiman

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kukataa vitendo hivyo, kutoa taarifa katika mamlaka husika na kuimarisha uwajibikaji katika maeneo mbalimbali ya jamii.