Dodoma FM

Wakazi Muungano walalamika kukosa huduma ya maji

2 November 2026, 17:47

Licha ya kuripoti mara kwa mara tatizo la uhaba wa maji bado tatizo hilo halija tatuliwa.Picha na IPP media.

Kukosa  huduma ya maji safi imepelekea wananchi hao kulazimika kuchangia vyanzo vya maji na mifugo.

Na Victor Chigwada.                                       

Wakazi wa vitongoji vya Wangama,  Kolimba na Kaunda Wilayani Chamwino wamelalamikia kuto fikiwa na huduma ya maji safi na salama hali inayo pelekea waendelee kutumia maji ya visima vya asili.

Wakizungumzia changamoto hiyo wananchi hao wamesema kukosa  huduma ya maji safi imepelekea wao kulazimika kuchangia vyanzo vya maji na mifugo.

Wamesema licha ya kuripoti mara kwa mara bado tatizo hilo halija tatuliwa hali inayo pelekea wananchi hao hususani wanawake kutumia muda mwingi kutafuta maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani.

Matonya Mtukamsihi mwenyekiti wa vitongoji hivyo katika Kijiji cha Muungano amesema adha hiyo ya maji ipo na hadi sasa hawaelewi itatatuliwa lini na mamlaka ya vijijini Ruwasa.

Ripoti ya Victor Chigwada.