Mitandao ya kijamii isiwakwamishe vijana kufanya shughuli za kujiingizia kipato
13 November 2026, 16:46

Beatrice Richard ambaye ni msindikaji wa mafuta ya alizeti kutoka Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma aliibuka mshindi na kukabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 4 ambazo zitakwenda kumsaidia kuongeza tija katika uzalishaji kutoka gunia 50 alizokuwa akizalisha kwa mwezi hadi gunia 100.
Na Victory Chigwada.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (Umwagiliaji), Athumani Kilundumya amewataka vijana kutumia muda mwingi zaidi katika kujizalishia mali badala ya kukesha kwenye mitandao ya kijamii bila ya manufaa kwao.
Kilundumya ameeleza hayo Novemba 12, 2026 wakati akifunga Programu ya ‘Generation Food Accelerator’ awamu ya pili ya Mradi wa Kilimo Biashara (VKB) unaotekelezwa na Shirika la Rikolto kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (WFP) pamoja na kukabidhi tuzo za vijana wabunifu wa mikoa ya Dodoma na Singida mkoani Dodoma jana.
Kwa upande wake Mratibu wa Miradi kutoka Rikolto, Shukuru Tweve aliwataka vijana hao wabunifu wanaoshiriki mradi huo kwenda kuwa mabalozi wa kuleta mabadiliko na kujenga biashara zenye tija na zenye kuhimili ushindani na zinazoweza kuchangia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.