Polisi Manyara yaanza operesheni dhidi ya bodaboda
5 October 2026, 17:04

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limetaganza oparesheni maalum ya kuwabaini na kuwakamata waendesha bodaboda wanaokiuka sheria za usalama barabarani, ikiwemo kuendesha kwa uzembe na kutofuata taratibu za usalama.
Na Kitana Hamisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani, amesema oparesheni hiyo inalenga kuhakikisha waendesha bodaboda wanazingatia sheria na taratibu za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.
Makarani amewataka waendesha bodaboda kuhakikisha wanakuwa na nyaraka muhimu, kutumia kofia ngumu na kuzingatia sheria zote za usalama barabarani, akisisitiza kuwa watakaobainika kufanya makosa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Amesema Jeshi la Polisi litaendelea kufanya oparesheni hizo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara na kuwataka waendesha bodaboda kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuzingatia sheria.