Umuhimu wa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii
19 November 2026, 16:46

Hivyo, utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii unapaswa kupewa kipaumbele na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanatumia teknolojia hiyo kwa usalama, uwajibikaji na manufaa ya maendeleo ya jamii.
Na Mwanaidi Mpetu.
Matumizi ya mitandao ya kijamii yameendelea kushika kasi katika jamii kutokana na maendeleo ya teknolojia, huku wananchi wengi wakiitumia katika kupata taarifa, kujifunza, kufanya biashara na kuwasiliana.
Matumizi yasiyo sahihi ya mitandao hiyo yamekuwa yakichangia changamoto mbalimbali ikiwemo kusambaa kwa taarifa za uongo, utapeli wa kimtandao na ukiukwaji wa faragha.
Baadhi ya wananchi wameeleza umuhimu wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, wakibainisha kuwa elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa watumiaji kuhusu namna bora ya kutumia majukwaa hayo.
Kwa upande wake, mtaalamu wa masuala ya Ustawi wa Jamii (Social Work) Salmin Mohammed ameeleza kuwa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ni muhimu katika kujenga jamii yenye uwajibikaji, maadili na uwezo wa kutambua madhara yanayoweza kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia.
Sauti ya Salmin Mohammed.