Wanaume wahimizwa kuhudhuria kliniki pamoja na wenza wao
26 October 2026, 17:39

Kwa mujibu wa miongozo ya afya ya uzazi nchini Tanzania ushiriki wa wenza hasa wanaume katika kliniki ya wajawazito una himizwa ili kuboresha afya ya mama na mtoto. Lengo ni kuhakikisha mwanaume anashiriki katika maandalizi ya kujifungua, anatambua dalili za hatari wakati wa ujauzito na anatoa msaada wa kiafya, kihisia na kifedha kwa mwenza wake.
Na Mariam Matundu.
Wanaume wameshauriwa kuhakikisha wanafika clinic na wake zao ili kuongeza ushiriki wa wanaume katika huduma za afya ya uzazi Pamoja na kupata ushauri Pamoja ili kumsaidia mama mjamzito kuwa na safari salama katika kipindi cha ujauzito.
Mkurugenzi msaidizi Idara ya afya ya uzazi mama na mtoto kutoka wizara ya afya Dkt Mzee Nasoro amesema kwa sasa serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ili kuwawezesha wanaume kuingia katika vyumba vya kujifungulia ili kumshuhudia mweza wake katika mchakato wa kuleta motto duniani.
Dkt Mzee amesema ili hatua ya kuwashirikisha wanaume katika suala la afya ya uzazi lifanikiwe kwa kiwango kikubwa ni muhimu wadau mbalimbali kutekeleza mpango huo.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Ihumwa jijini Dodoma wanaunga mkono suala la wanaume kuhudhuria clinic na wenza wao kwani wamesema kuna faida nyingi.