Dodoma FM

Uelewa mdogo wa jamii wachelewesha matibabu ya Selimundu kwa watoto

2 September 2026, 17:17

Licha ya maendeleo makubwa katika sekta ya afya nchini Tanzania, changamoto ya uelewa duni miongoni mwa wananchi imesalia kuwa kikwazo.Picha na Mtandao.

Duniani kote, Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa hadi kufikia mwaka 2021, takribani watu milioni 7.74 walikuwa wanaishi na ugonjwa huu, huku asilimia 80 ya wagonjwa wote wakipatikana katika nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwemo Tanzania.

Na Husna Munis.

Wataalamu wa afya nchini wametahadharisha kuwa ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell) unazidi kuwa tishio kwa afya ya watoto na ustawi wa familia, huku uelewa mdogo wa jamii ukitajwa kuchangia watoto wengi kugundulika wakiwa tayari wamepata madhara makubwa.

Licha ya maendeleo makubwa katika sekta ya afya nchini Tanzania, changamoto ya uelewa duni miongoni mwa wananchi imesalia kuwa kikwazo kikubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa kurithi.

Mtaalamu na mshauri wa masuala ya afya kutoka kliniki ya Blessed Team Daktari Nelson Wiston Mfumya, ametoa wito kwa jamii kuchukua hatua mapema ili kupambana na ugonjwa huu.

Akifafanua kitaalamu kuhusu ugonjwa huo, Daktari Mfumya ameeleza kuwa ugonjwa wa seli mundu hutokea pale chembe nyekundu za damu zinapobadilika muundo wake wa kawaida.

Ili kufahamu hali halisi ya uelewa wa ugonjwa huu katika ngazi ya jamii, KM24 imezungumza na baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mama Farida,katika kata ya Nyasubi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambao wameeleza mitazamo na uelewa wao kuhusu ugonjwa huo wa selimundu.

Sauti ya Husna kina.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Tanzania, inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 20 ya watanzania wamebeba kinasaba cha ugonjwa huu bila wao kuugua, huku takribani watoto 11,000 wakizaliwa na seli mundu kila mwaka nchini.