Dodoma FM

Uwekezaji wa kifedha watajwa kuwa muhimu kufikia malengo

4 September 2026, 16:33

Wananchi washauriwa kuzingatia ushauri kabla ya kufanya uwekezaji wa kifedha ili kufikia malengo yao waliyojiwekea. Picha na mtandao.

Mtaalamu na mshauri wa masuala ya kifedha Bwana Thobias Swai,wananchi kuwa na fedha halali na kutafuta maeneo sahihi ya kuwekeza, ikiwemo benki, hisa, biashara, mashamba, majengo na mali zisizohamishika, huku akisisitiza umuhimu wa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na taasisi husika kabla ya kuwekeza.

Na Daniel Njau.

Uwekezaji wa kifedha umetajwa kuwa muhimu katika kufikia malengo ya kiuchumi, huku wananchi wakishauriwa kufanya utafiti na kuzingatia gharama kabla ya kuamua eneo la kuwekeza fedha zao.

Baadhi ya wananchi wamesema wamekuwa wakijifunza kwa watu waliofanikiwa, kutumia elimu wanayopata darasani katika maisha ya kila siku, pamoja na kuchambua gharama na faida kabla ya kuingia kwenye uwekezaji.

Hata hivyo, wamesema baadhi ya watu hukosa ubunifu na kuamua kufanya biashara zinazofanywa na watu wengi katika eneo moja, hali ambayo inaweza kuongeza ushindani na kupunguza uwezekano wa kupata faida katika uwekezaji.

Sauti na Daniel Njau.