Dodoma FM

Wakazi chinyika walia uhaba wa maji

21 August 2026, 17:31

Uhaba wa maji katika kitongoji cha chinyika ng’ahelezi na kumepelekea wakazi wa eneo hilo kutumia maji ya Korongo. Picha na mtandao.

Msafiri Chahonza mwenyekiti wa Kijiji Cha Ng’ahelezi amesema vipo vitongoji zaidi ya kimoja ambavyo havina huduma ya maji huku baadhi ya vitongoji hivyo vikikabiliwa na uhaba wa miundombinu ya mabomba ya maji.

Na Victor Chigwada.                          

Uhaba wa maji katika kitongoji cha Chinyika Ng’ahelezi Wilayani Chamwino kumepelekea wakazi wa eneo hilo kutumia maji ya Korongo ambayo si safi na salama.

Wananchi wa Chinyika wamesema kuwa maji ya bomba kwao imabaki kama hadithi isiyo na matumaini licha ya dhamira ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani lakini kwao bado imekuwa tofauti hivyo wameiomba serikali kutatua kero hiyo.

Sauti na Victor Chigwada.