Dodoma FM

Elimu ya awali msingi bora wa kumuandaa mtoto

1 September 2026, 16:54

Elimu ya awali huwasaidia watoto kupata msingi wa kujifunza kabla ya kuingia darasa la kwanza.Picha na Mtandao.

Hata hivyo, ubora wa elimu ya awali ni muhimu. UNICEF imeeleza kuwa baadhi ya watoto wanaweza kuingia darasa la kwanza bila kuwa wamepata maandalizi yakutosha endapo elimu ya awali wanayopewa haina ubora unaostahili.

Na Crispine Gerald.

Imeelezwa kuwa elimu ya awali, ni muhimu katika maendeleo ya mtoto kabla ya kuanza elimu ya msingi kwani Kupitia elimu hiyo, mtoto hujifunza stadi za awali za kusoma, kuandika, kuhesabu, kushirikiana na wenzake pamoja na kujenga uwezo wa kujifunza.

Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, elimu ya awali inalenga kumkuza mtoto kimwili, kiakili, kihisia na kijamii, ikiwa ni pamoja na kumuandaa kujiunga na elimu ya msingi.

Baadhi ya wazazi wanaeleza maoni yao kuhusu elimu ya awali inawasaidia watoto kuwa tayari wanapoanza darasa la kwanza, wakitaja mabadiliko wanayoyaona kwa watoto wao baada ya kupitia elimu hiyo.

Sauti za wazazi

Mwalimu Jamila Masi mwalimu wa shule ya msingi Makole jijini Dodoma yeye anasema elimu ya awali huwasaidia watoto kupata msingi wa kujifunza kabla ya kuingia darasa la kwanza.

Anasema kupitia michezo na shughuli mbalimbali za kujifunza, watoto hujenga stadi za msingi za kusoma, kuandika, kuhesabu na kushirikiana na wengine.

Sauti ya Mwalimu.

Utafiti wa UNICEF kuhusu ujifunzaji wa awali Tanzania unaonyesha kuwa elimu bora ya awali inaweza kusaidia kuongeza utayari wa mtoto kuanza elimu ya msingi.