Dodoma FM
Dodoma FM
5 May 2025, 18:14

Wakazi wa kijiji hicho wameiomba serikali iwasaidie ujenzi wa bweni ili kuwanusuru watoto na vitendo hivyo vya ukatili.
Na Kitana Hamis.
Suzana Samweli Mwenye umri wa Miaka 13 Mwanafunzi wa Darasa la Sita amefariki Dunia Baada ya kubakwa na Kuuwawa Kisha kutobolewa Macho. katika Kijiji cha Gedamara kata ya Galapo wilayani Babati mkoani Manyara.
Tukio hilo limetokea April 29 ambapo baada ya tukio hilo mwili wa binti huyo ulitupwa katika shamba la mbaazi.
Wakazi wa kijiji hicho wameiomba serikali iwasaidie ujenzi wa bweni ili kuwanusuru watoto na vitendo hivyo vya ukatili
Kamanda wa polis mkoa wa Manyara Ahemd Makarani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amekiri kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi huku uchunguzi mwingine ukiendelea.