Maafisa usafirishaji watakiwa kuzingatia sheria
8 July 2026, 16:03

Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, hadi mwaka 2026 zaidi ya waendesha bodaboda na bajaji 209,632 walikuwa wamerasimishwa kupitia mifumo ya Serikali.
Na Bennard Komba.
Maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya nchi katika utekelezaji wa shughuli zao badala ya kushawishiwa na makundi yanayo weza kuhatarisha amani na utulivu.
Wito huo unakuja kufuatia mtazamo uliopo kwa baadhi ya wananchi kwamba baadhi ya waendesha bodaboda wamekuwa wakihusishwa na vitendo vinavyo vuruga amani.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Usafirishaji wa bodaboda na Bajaji Mkoani Dodoma, Issa Rashid Swai, amesema jukumu la umoja huo ni kuwahamasisha wanachama kuheshimu sheria za nchi na kufanya kazi kwa weledi.
Ameongezakuwasektayabodabodanabajajiimeendeleakuwachanzomuhimu cha ajirakwavijanawengi, huku sera zilizopozikitoafursakwa wananchi kujiajirikupitiashughulihiyo.
Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, hadi mwaka 2026 zaidi ya waendesha bodaboda na bajaji 209,632 walikuwa wamerasimishwa kupitia mifumo ya Serikali.
Aidha, waendesha bodadoda na bajaji 4,109 walikuwa wamesajiliwa kupitia mfumo wa WBN-MIS, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuirasimisha na kuimarisha sekta hiyo.