Dodoma FM

Wananchi Muungano wapongeza uboreshaji wa miundombinu chakavu ya maji

26 May 2026, 17:15

Uchakavu wa miundombinu ya maji ulipelekea uhaba wa maji wa mara kwa mara ila kwa sasa wamepata mafundi.Picha na Mtandao.

Awali mabomba hayo yalikuwa yakipasuka na kupelekea maji kukosekana  kijijini hapo hali iliyo walazimu wakazi wa eneo hilo kuchota maji katika visima.

Na Victor Chigwada.

Kuimarishwa kwa huduma ya miundombinu ya maji katika kijiji cha Muungano wilayani chamwino kumeleta ahueni kwa wakazi wa eneo hilo ambapo uchakavu wa mabomba ulipelekea ukosefu wa maji mara kwa mara.

Akiongea na Taswira ya habari mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Matonya Mtukamsihi amesema kuwa uchakavu wa miundombinu ya maji ulipelekea uhaba wa maji wa mara kwa mara ila kwa sasa wamepata mafundi ambao wamrekebisha chanagamoto hiyo na huduma za maji zimerejea .

Aidha Mtukamsihi  ameiomba mamlaka ya maji kuongea mabomba ya maji katika eneo hilo ili kupunguza foleni na pia wanahitaji tenki lenye ujazo mkubwa kwaajiliya kuhifadhi maji kijijini hapo.

Sauti ya Matonya Mtukamsihi.

Imeelezwa hapo awali mabomba hayo yalikuwa yakipasuka na kupelekea maji kukosekana  kijijini hapo hali iliyo walazimu wakazi wa eneo hilo kuchota maji katika visima ili kukidhi mahitaji yao.

Sauti za wananchi.