Dodoma FM

Wananchi Nguji kuondokana na tatizo la huduma za afya

6 April 2023, 2:29 pm

Muonekano wa zahanati hiyo ya Nguji ikiwa katika ukarabati. Picha na Bernad Magawa.

Jengo la zahanati ya nguji ni miongozi mwa majengo mapya zaidi ya saba ya kutolea huduma za afya yanayoendelea kujengwa wilayani Bahi.

Na Bernad Magawa.

Wananchi wa kijiji cha Nguji wilayani Bahi wanatarajia kuondokana na tatizo la kukosa huduma za afya pindi zahanati inayojengwa kijijini hapo itakapo kamilika mapema mwaka huu.

Wananchi wa nguzji ambao wamekuwa wakifuata huduma za afya zaidi ya kilomita kumi na mbili kwenye kijiji Mundemu, kwa kushikiana na serikaali pamoja na Mbunge wa jimbo la Bahi kupitia mfuko wa jimbo, wamejenga zahanati ambayo kwa sasa ipo katika hatua za umaliziaji.

Akizungumza kuhusiana na ujenzi huo kaimu afisa mtendaji kijiji cha Nguji Mwalimu Mathias Nziku amesema zaidi ya shilingi million 78 zimetumika katika ujenzi huo ambao kukamilika kwake kutawaletea nafuu wananchi wa Nguji hususa ni akina mama wajawazito na watoto ambao hupata adha kubwa wakati wanapohitaji huduma ya mama na mtoto.

Sauti ya Kaimu afisa mtendaji kijiji cha Nguji.
Muonekano wa jengo la zahati hiyo. Picha na Bernad Magawa.

Naye kaimu Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bahi Honolina Mnkunda akizungumza kuhusiana na kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo amesema kwa mwaka 2023 halmashauri kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato ya ndani inatarajia kumalizia baadhi ya majengo ya zahanati ikiwemo zahanati ya nguji ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Bahi.

Imeelezwa kuwa Jengo la zahanati ya nguji ni miongozi mwa majengo mapya zaidi ya saba ya kutolea huduma za afya yanayoendelea kujengwa wilayani Bahi ambapo kukamilika kwa majengo hayo kutaiwezesha wilaya ya Bahi kufikisha huduma za afya kwa wananchi wote wilayani humo.