Dodoma FM

Serikali yatatua kero ya maji Mvumi Misheni

20 January 2023, 3:12 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Mvumi misheni Wilayani Chamwino wameipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa juhudi za kutatua changamoto ya maji

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema kuwa kujengwa kwa mradi  huo wa  maji katika Kata yao utasaidia kukomesha changamoto hiyo

Alpha Zoya ni mwenyekiti wa kijiji cha Mvumi amekiri hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwasasa inatoa matumaini kutokana na mradi mkubwa wa ujenzi na uchimbaji wa visima vya maji

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Bw.Aidani Lubeleje amekiri  kuwa kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya upatikanji wa huduma ya maji

Amesema kutokana na mradi huo wanategemea hivi karibuni kuondokana na adha hiyo