Dodoma FM

Vitunguu kupanda bei , baada ya msimu wake kwisha

21 April 2021, 10:27 am

Na; Tosha Kavula.

Imeelezwa kuwa uchache wa zao la vitunguu sokoni hivi sasa, unasababishwa na msimu wake wa mavuno kupita.

Wakizungumza na Dodoma Fm wafanyabiashara wa zao hilo katika soko la Majengo wamesema hali hii imechangia bei ya zao hilo kupanda na kushuka.

Aidha wanunuzi wa zao hilo wameomba kushushiwa bei  kwa kuwa hadi sasa mteja hawezi kupata vitunguu vya shilingi mia tano kama ilivyokuwa awali.

Upatikanaji wa vitunguu kwa sasa umekuwa wa wastani kutokana na msimu wake kupita,na wanunuzi wengi wametoa wito bei kupungua ili waweze kuimudu.