Dodoma FM

Wajasiriamali waeleza kunufaika na wiki ya ubunifu

27 April 2023, 6:42 pm

Maonyesho ya wiki ya ubunifu yanaendelea katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Picha na Thadei Tesha.

Katika maenesho hayo dodoma tv imeshuhudia bidhaa mbalimbali ambazo zimebuniwa na wajasiriamali pamoja na wanafunzi wabunifu kutoka katika tasisi mbalimbali ambapo wanatumia fursa hiyo katika kuzionyesha kwa jamii katika maonesh ya wiki ya ubunifu maarufu kama MAKISATU.

Na Thadei Tesha.

Wakati maonyesho ya wiki ya ubnifu yakiendelea kufanyka katika uwanja wa jamhuri jijini dodoma baadhi ya wajasiriamali wameelezea namna walivyonufaika kufuataia uwepo wa maonyesho hayo.

Dodoma tv imewatembele a na kufanya mahojiano na baadhi ya wajasriamali ambao pia ni wabunifu wa bidhaa mbalimbali ambapo hapa wanaanza kwa kuelezea juu ya bidhaa wanazozalisha pamoja na uwepo wamaonsho hayo yanavyosaidia kukuza bunifu zao.

Sauti za Wajasiriamali.
Baadhi ya bidhaa zilizo buniwa na kutengenezwa na wabunifu hao. Picha na Thadei Tesha.

Aidha baadhi ya wajasiriamali hao wameongeza kuwa ili kusaidia wjasiriamali wengi kuzidi kukua katika bunifu zao ni vyema seriakali kutoa kipaumbele katika maonesho mbalimbali yanayofanyika ikia ni pamoja na kuwapa mahema maalum na sio kwa taasisi pekee.

Sauti za wajasiriamali.