Dodoma FM

Kipindupindu chatajwa kuwakumba wanawake zaidi nchini

29 January 2024, 8:00 pm

Picha ni baadhi ya wanahabari wa jijini Dodoma ambao walihudhuria leo katika MEDIA SCIENCE CAFEE iliyofanyika ukumbi wa Cavillam jijini Dodoma. Picha na Mariam Kasawa.

Kipindupindu unatajwa kuwa ugonjwa hatari ambao huambatana na kuharisha na kutapika huku ikielezwa kuwa ni asilimia 10 tu ya wagonjwa wanaopata kipindupindu na kulazwa hospitali huku wengine wakitembea na vimelea vya ugonjwa huo.

Na Mariam Matundu.
Wanawake nchini Tanzania wanatajwa kuongoza kwa asilimia 49.6 kupata maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu kutokana na shughuli mbalimbali wanazozifanya.

Wakati ikielezwa kuwa kipindupindu huashiria hali ya umasikini huku ukubwa wa tatizo la mlipuko wa ugonjwa huo ukitajwa kuchukua takribani million 1.3 ya nchi duniani na Tanzania ikiwemo.

Bi. Theresia Masoi ni mtafiti kutoka chuo kikuu cha Dodoma hapa anaelezea maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huu huku akieleza zaidi ni kwanini wanawake wamekuwa wahanga wakubwa wa ugonjwa huu.

Sauti ya Bi Theresia Masoi ni Mtafiti kutoka chuo kikuu cha Dodoma.
Picha ni Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Bi Rose Reuben akiongea na washiriki wa MEDIA SCIENCE CAFEE wakati akihitimisha . Picha na Mariam Kasawa.

Umuhimu wa kupanga bajeti ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu nao unatajwa kuwa nuhimu zaidi hususani kwa serikali kama anavyoeleza Bw. France Lasway mchumi kutoka Wizara ya Afya .

Sauti ya Bw. France Lasway mchumi kutoka wizara ya Afya .

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Bi Rose Reuben akapata wasaa wa kuilezea kwa ufupi maana ya MEDIA SCIENCE CAFEE ambayo imekuwa ikiwakutanisha waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali .

Sauti ya Bi Rose Reuben Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA
Picha ni Bw. France Lasway mchumi kutoka wizara ya Afya akizungumzia umuhimu wa kupanga bajeti kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko.Picha na Mariam Kasawa.