Dodoma FM

Wamiliki wa maabara watakiwa kusimamia ubora wa maabara zao

7 December 2021, 11:05 am

Na; Shani Nicolous.

BODI ya Maabara Binafsi za Afya (PHLB) nchini inawasisitiza wamiliki na wataalamu wa maabara kote nchini, kusimamia ubora wa maabara zao ili kuleta huduma sahihi katika jamii.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi za Afya nchini Dominic Fwiling’afu ambapo amesema kuwa uamuzi wa tiba sahihi ya mgonjwa hutegemea majibu sahihi ya vipimo vya uchunguzi wa Maabara.

Fwiling’afu amewataka wamiliki na wataalamu wa maabara Kote nchini kuzingatia Miongozo mbalimbali ya bodi katika kuhakikisha huduma zinazotolewa kwenye maabara binafsi zinakuwa na viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

Wananchi wametoa maoni yao juu ya hili ambapo wamesema jamii isichukulie urahisi wa kumiliki maabara bila kufuata sheria hii itasaidia kutokomeza huduma duni katika baadhi ya maabara nchini.

Usajili wa Maabara binafsi ya afya nchini unafanywa kisheria kupitia kifungu cha 14 na 15 vya Sheria ya Maabara Binafsi,Kifungu cha 14(1) kinatoa katazo kwamba mtu yeyote hata paswa kufanya shughuli za maabara binafsi hadi mtu huyo awe amesajiliwa kupitia kifungu hiki.