Dodoma FM

Ujenzi wa shule katika Mtaa wa Mbwanga kuinua kiwango cha elimu

28 December 2023, 10:04 pm

Wakazi wa Mtaa huo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule hiyo.Picha na Mariam Matundu.

Afisa Mtendaji wa mtaa huo ameahidi kuhakikisha hakuna mtoto anae achwa nyuma katika zoezi la uandikishaji wa darasa la kwanza na awali.

Na Mariam Matundu.
Kukamilika kwa ujenzi wa shule ya Msingi Jitegemee ilijengwa katika Mtaa Mbwanga kata ya Mnadani kunatarajia kuinua kiwango cha elimu katika kata hiyo.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi katika kata hiyo ambapo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule hiyo ambapo wamesema awali wanafunzi walipata shida kutokana na umbali mrefu kufuata shule katika kata za jirani ikiwemo Chang’ombe.

Sauti za wananchi.
Picha ni muonekano wa shule hiyo iliyojengwa katika mtaa wa Mbwanga kata ya mnadani . Picha na Mariam Matundu.

Nae Afisa Mtendaji wa kata ya Mnadani Bi. Caroline Masawe ameshukuru kwa kukamilika kwa mradi huo huku akiahidi kusimamia ipasavyo hasa suala la uandikishaji wa wanafunzi amabao wanatarajia kuanza masomo mwakani ili kuhakikisha hakuna mtoto katika kata hiyo anaechwa nyuma.

Sauti ya Afisa mtendaji.