Dodoma FM

Kiteto wakumbwa na hofu eneo la makaburi kujaa

14 May 2025, 1:55 pm

Picha ni eneo la makaburi wilayani humo ambapo inadaiwa eneo la kuzika limebaki dogo sana hivyo wananchi wanahitaji kutengewa eneo jipya.Picha na Kitana Hamis.

Hofu imetanda miongoni mwa wakazi wa eneo hilo kwani wananchi wanadai kuwa hakuna eneo mbadala.

Na Kitana Hamis.
Wakazi wilayani Kiteto mkoani Manyara wahofia kukosa maeneo ya kuzika kutokana na eneo la makaburi kujaa.

Hofu imetanda miongoni mwa wakazi wa eneo hilo kwani wananchi wanadai kuwa hakuna eneo mbadala lililo andaliwa ambalo litatumika kwaajili ya makaburi.

Baadhi ya Wananchi Mjini Kibaya wilayani humo wakizungumzia na taswira ya Habari wameiomba Serikali kuwasaidia kutenga maeneo Mengine kwajili ya kuhifadhi wapendwa wao pindi wanapo fariki huku kiongozi wa Dini ya Kislamu Saidi Salmu anaeleza hali ilivyo na jitihada walizo chukuwa hadi sasa.

Sauti za wananchi.