Dodoma FM

Leo tunaangazia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

27 November 2023, 5:44 pm

Picha ni Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalum dkt Dorothy Gwajima. Picha na Green waves media.

Hatua za kutokomeza ukatili zianzie katika ngazi ya familia.

Na Mwandishi wetu.

Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia imezinduliwa ikiwa na kauli mbiu isemayo wekeza kutokomeza ukatili ,kaulimbiu ambayo imewaleta wadau ,serikali na famili kwa pamoja katika kutafakari na kuwekeza katika kuzuia ukatili wa kijisia .

waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalum dkt Dorothy Gwajima ametaka hatua za kutokomeza ukatili zianzie katika ngazi ya familia.