Wazazi watakiwa kuunga mkono mpango wa chakula shuleni
31 July 2026, 17:35

Baadhi ya wazazi wamesema uwepo wa chakula shuleni ni kuimarisha taaluma ya shule Kwa ujumla hivyo upo umuhimu wa Kila mzazi kushiriki, tofauti na hapo Sheria zichukuliwa Kwa wazazi wanao kaidi sanjali na kuendelea kuwa elimisha wananchi juu ya umuhimu wa chakula shuleni.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Makang’wa wametakiwa kuachana na mawazo hasi yanayo kwamisha wao kuchangia chakula shuleni.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Aidani Mamba amesema tangu mwaka Jana walikubaliana kuchangia chakula cha watoto shuleni licha ya baadhi Yao kuendelea kusuasua juu ya uchangiaji huo.
Mamba amewasihi wazazi kutoa mchango huo kwani ni faida ya mtoto wake ambaye atanufaika na kupanda kielimu kwa kushirikiana na wenzake Kwa muda mrefu