Dodoma FM

Matumizi ya huduma ya maji kielektroniki suluhisho kwa wananchi miyuji

27 August 2026, 17:03

Matumizi ya teknolojia yakitoa fursa ya kufanya huduma ya maji kuwa rahisi na ufanisi zaidi. Picha na mtandao.

Huduma hiyo inaendelea kuwa sehemu ya juhudi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa jamii, huku matumizi ya teknolojia yakitoa fursa ya kufanya huduma hiyo kuwa rahisi na yenye ufanisi zaidi.

Na Elizabeth Mwinuka.                                                    

Katika kuhakikisha jamii inapata maji safi na salama, matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa huduma za maji yameendelea kuwa suluhisho kwa wananchi, hususani katika maeneo yenye changamoto za upatikanaji wa maji

Wakazi wa Kata ya Miyuji jijini Dodoma wameeleza kuwa huduma ya maji safi inayotolewa kupitia mfumo wa kielektroniki imewarahisishia upatikanaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani, huku wakisema huduma hiyo imepunguza gharama na changamoto za kutafuta maji salama.

Kwa upande wake, wakala wa huduma hiyo Suzanna Anjelist ameeleza namna mfumo wa kielektroniki unavyofanya kazi na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ufanisi nafaida za matumizi ya maji yanayopatikana kupitia mfumo huo.

Sauti na Elizabeth Mwinuka.