Dodoma FM

PSPTB yawataka wataalam kulipa madeni ndani ya siku 30

15 September 2026, 09:03

Mtendaji wa PSPTB, Godfred B. Mbanyi, akitoa agizo la wataalam wa PSPTB kulipa madeni ndani ya muda uliowekwa. Picha na Anwary Shabani.

Mtendaji wa PSPTB Bwana Godfred Banyi amewasihi wataalamu wote wa PSPTB wenye madeni kutumia fursa hiyo ya siku 30 kulipa ada zao kwa wakati ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza katika usajili na shughuli zao za kitaalamu.

Na Anwary Shabani.

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi, imewataka wataalamu wa  PSPTB wenye madeni ya ada za mwaka za usajili kuhakikisha wanalipa madeni hayo ndani ya siku 30, huku ikionya kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bodi.

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfred B. Mbanyi, kupitia tangazo la Bodi, akiwataka wataalamu ambao hawajakamilisha malipo ya ada zao kutimiza wajibu huo ndani ya muda uliowekwa.

Mbanyi amesema mtaalamu yeyote atakayeshindwa kulipa deni lake ndani ya siku 30 anaweza kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bodi, ikiwamo hatua zinazoweza kuathiri hadhi ya usajili wake.

Simulizi na Anwary Shabani.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema majina ya wataalamu wote ambao watakuwa wamekamilisha malipo yao na hawana madeni yatachapishwa kwenye Gazeti la Serikali pamoja na tovuti rasmi ya PSPTB.