Dodoma FM

Vitongoji vya Dabalo vyaiomba serikali kuwafikishia umeme

1 October 2026, 17:29

Picha ni zoezi la usambazji wa umeme katika maeneo ya vijijini likiendele na wananchi kiunufaika. Picha na Mwananchi.

Wananchi hao wameiomba Serikali kuwafikishia umeme ili kuwezesha huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi, huku wakieleza kuwa ukosefu wa nishati hiyo unakwamisha fursa za uzalishaji na ujasiriamali.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa vitongoji vya Chikwama, Mbande na Majengo, Kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, wameiomba Serikali kuwafikishia huduma ya umeme ili kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi zinazotegemea nishati hiyo.

Wamesema ukosefu wa umeme umesababisha baadhi ya huduma ndogondogo, ikiwemo mashine za kusaga nafaka, kutopatikana, huku vijana wakikosa fursa za kuanzisha shughuli za uzalishaji kama karakana za kuchomelea, hali wanayodai inakwamisha maendeleo ya vitongoji hivyo.

Diwani wa Kata ya Dabalo, Omary Kiguna, amesema licha ya vijiji vyote katika kata hiyo kufikiwa na umeme, changamoto bado ipo katika vitongoji, ambapo karibu nusu ya vitongoji 34 havijafikiwa na huduma hiyo.

Kiguna amesema baadhi ya vitongoji tayari vimejumuishwa katika mpango wa kupelekewa umeme, ikiwemo Mbande, Majengo na Chikwama.

Simulizi na Victor Chigwada.