Wazazi wahimizwa kuwapeleka watoto kupata chanjo ya Polio
2 November 2026, 18:02

Wazazi jiji dodoma wazazi wametakiwa kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata chanjo ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Polio na kuchangia juhudi za kuutokomeza ugonjwa huo. hayo wakati wa matembezi yaliyoandaliwa na Rotary Club of Mwalimu Nyerere Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa Polio duniani.
Na Anwary Shabani.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata chanjo ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Polio na kuchangia juhudi za kuutokomeza ugonjwa huo.
Amesisitiza kuwa chanjo ni muhimu kwa afya na usalama wa watoto, huku akiwahimiza wazazi kutumia fursa ya huduma hizo zinazotolewa bure badala ya kupuuza umuhimu wake.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa matembezi ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo ya Polio yaliyoandaliwa na Rotary Club of Mwalimu Nyerere Dodoma.
Rais wa Rotary Club of Mwalimu Nyerere Dodoma, Kathrin Mwembekam, amesisitiza umuhimu wa kuungana na wadau mbalimbali duniani katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu ugonjwa wa Polio na kuhamasisha juhudi za kuutokomeza.
Naye mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) amesema elimu kuhusu ugonjwa wa Polio ndiyo iliyomhamasisha kushiriki katika matembezi hayo, huku akitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa huo.
maelezo hayo wakati wa matembezi yaliyoandaliwa na Rotary Club of Mwalimu Nyerere Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa Polio duniani.