Wananchi waiomba TANESCO kupunguza gharama za umeme
22 October 2026, 12:57

Utaratibu huo unalenga kumkomboa mwananchi asiye na uwezo wa kulipia gharama za kuvuta umeme au kulipia nguzo za umeme.
Na Victor Chigwada.
Wakazi jijini Dodoma wameiomba Serikali kupitia shirika la umeme nchini TANESCO kupunguza gharama za kuvuta umeme Kwa wananchi ili kuwanufaisha wengi na kuongeza mapato .
Pamoja na kutoa pongezi kwa Serikali juu ya usambazaji wa Nishati ya umume Wananchi hao wameonesha nia ya uzalendo ya kuhakikisha kila mwananchi anabeba jukumu la kulipia Kodi ya jengo ambayo kwasasa inakatwa kupitia manunuzi ya token za umeme(luku).
Wamesema ili zoezi la ulipaji kodi wa majengo lifanyike kwa urahisi na kwa kila mwananchi anae miliki nyumba ni vema serikali ikafikiria kupunguza gharama za kuvuta umeme .
Naye Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma Mhandisi Donasiano Shamba mewatoa shaka wananchi hao ambapo amesema kuwa tayari Serikali kwa kushirikiana na benki ya CRDB wapo katika hatua za makubaliano ya kutoa mikopo ya kuunganishiwa huduma ya umeme Kwa wananchi wote.
Shamba ameongeza kuwa utaratibu huo unalenga kumkomboa mwananchi asiye na uwezo wa kulipia gharama za kuvuta umeme au kulipia nguzo za umeme atawezeshwa na benki hiyo huku upande wa vijiji mradi huo utatolewa bure Kwa kuunganishiwa umeme.