Wanaume wahimizwa kushiriki kutokomeza ukatili katika jamii
2 November 2026, 16:44

Amesisitiza kuwa jukumu la kumlinda motto na kumpa malezi bora halipaswi kuachiwa mzazi mmoja, bali linahitaji ushirikiano wa wazazi wote wawili, walezi na jamii nzima ili kujenga kizazi kinacho heshimu haki na usalama wa wengine.
Na Daniel Njau.
Vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto vimeendelea kuwa changamoto katika jamii, huku wanaume wakihimizwa kutumia nafasi zao kama walezi, walimu na walinzi kushiriki kikamilifu katika kupinga na kutokomeza vitendo hivyo.
Baadhi ya wananchi wamesema wanaume wana nafasi muhimu katika kujenga jamii salama kwa kushirikiana na wazazi, walezi na jamii kwa ujumla katika kutoa malezi bora na kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya ukatili.
Mlezi wa kituo cha watoto cha Esses Children, Bi Lea Mtalali, amesema ushiriki wa wanaume katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ni muhimu, akibainisha kuwa baadhi yao wamekuwa wakiacha jukumu la malezi kwa wanawake pekee, badala ya kusimama katika nafasi zao kama baba na walezi.
Ameeleza kuwa watoto wanao kulia katika mazingira ya unyanyasaji wanaweza kuathirika kisaikolojia na kujenga tabia za ukatili wanapokuwa watu wazima, hivyo wazazi wanapaswa kushirikiana kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama.