Dodoma FM

Wananchi wanawezaje kukabiliana na gharama za maisha?

10 September 2026, 16:38

Ni muhimu wananchi kuweka akiba kulingana na uwezo wao, kupanga matumizi sahihi ili kufikia malengo yao. Picha na mtandao.

Akizungumza kuhusu namna ya kukabiliana na hali hiyo, Mshauri wa Masuala ya Kifedha, Bwana Joel Mkede, amesema ni muhimu wananchi kuweka akiba kulingana na uwezo wao, kupanga matumizi na kuanza na mahitaji muhimu kama chakula, huku wakiepuka matumizi yasiyo ya lazima.

Na Daniel Njau.

Wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kuweka akiba ya fedha na kupanga matumizi ya msingi ili waweze kukabiliana na ongezeko la gharama za maisha, hasa pale bei za bidhaa na huduma zinapopanda.

Baadhi ya wananchi wanasema hali ya kipato na mahitaji mbalimbali ya kila siku imekuwa changamoto, hali inayowafanya kushindwa kuweka akiba na hivyo kupata ugumu wa kumudu gharama za maisha zinapoongezeka.

Sauti na Daniel Njau.