Dodoma FM

Je unashiriki vipi kutunza miundombinu ya barabara katika eneo lako

18 April 2024, 5:45 pm

Picha ni moja kati barabara zinazo jengwa katika jiji la Dodoma.Picha na Thadei Tesha.

Serikali kupitia wakala wa barabara Nchini TANROADS wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kupitia majukwaa mbalimbali juu ya ushiriki wa wananchi katika utunzaji wa miundombinu ya barabara Nchini jambo ambalo linapaswa kutekelezwa na kila mwananchi.

Na Thadei Tesha.
Seriali imeendelea na juhudui za kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ikiwemo Jiji la Dodoma lengo ikiwa ni kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.

Pamoja na kukamilika kwa miundombinu hiyo lakini kumekuwa na changamoto ya baadhi ya miundombinu hiyo kuharibika huku mingine ikisabaishwa na wananchi.

Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya wananchi Jijini Dodoma kufahamu namna elimu ya utunzaji wa miundombinu ya barabara wanavyoitumia kuhakikisha inaendelea kuleta manufaa kwa jamii kama ilivyokusudiwa.

Sauti za wananchi.